Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji

Hon. George Joseph Kakunda (Mb)

Wasifu

Ziara ya Waziri Mkoani SIMIYU wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charl;es Mwijage Mkoani Simiyu.


Imewekwa: 03rd January, 2018

ZIARA YA WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI MHE. CHARLES MWIJAGE MKOANI SIMIYU, TAREHE 2/01/2018, WAKATI WA UFUNGUZI WA OFISI ZA SIDO NA KUKABIDHI ENEO KWA MKANDARASI KWA AJILI YA UJENZI WA ENEO LA VIWANDA. Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage afanya Ziara katika mkoa wa Simiyu leo tarehe 2/1/2018. Katika ziara yake Mhe. Mwijage amekutana na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka na kufanya mazungumzo mafupi kabla ya kushiriki zoezi la ufunguzi wa ofisi za SIDO mkoa wa Simiyu. Mara baada ya Ufunguzi wa Ofisi hizo Mhe. Waziri alipata furesa ya kuzungumza machche na kutoa maagizo ya Utekelezaji. Kwanza alianza kwa kuupongeza uongozi wa SIDO kwa kujenga Ofisi hizo ambapo ameagiza kuwepo madarasa maalumu ya mafunzo kwa vitendo. Mhe. Waziri amesema “Uchumi wa Viwanda utajengwa na Viwanda vidogo hivyo Uzinduzi wa ofisi hizi za SIDO ndio chachu ya maendeleo ya Viwanda katika Mkoa wa SIMIYU” Aidha Mhe. Waziri alitembelea eneo la Viwanda na kukabidhi eneo hilo kwa Mkandarasi ambaye anatakiwa kujenga kwa haraka ili watanzania wapate fursa ya kuanzisha Viwanda. Pia Waziri alihitimisha ziara yake kwa kuklutana na Viongozi wa Serikali, Vipongozi wa Dini, Viongozi wa Vyama, Wawekezaji na Wafanyabiashara na kuzungumza nao juu ya Serikali ya awamu ya tano ilivyojipanga katika kuendeleza Viwanda nchini. Mhe. Waziri alieleza kuwa, wananchi wa Mkoa wa Simiyu sasa watapata fursa za kuwekeza, kufanya biashara, waatapata ajira pamoja na mikopo nafuu mara baada ya ujenzi wa eneo la Viwanda. Mhe. Waziri alieleza kuwa kujenga uchumi wa Viwanda ambao ni shughuli ya kiujumla inayomtaka kila mmoja kushiriki katika kuhakikisha tunafanikisha adhma ya kuwa nchi ya Viwanda ifikapo mwaka 2025. Pia aliongeza kuwa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji ndiyo injini ya mafanikio katika uchumi kwa vile uchumi wa nchi yoyote hubebwa na Viwanda ambavyo huzalisha bidhaa zitokanazo na malighafi zinazozalishwa sehemu husika na kutumika katika eneo husika. Mhe, Waziri amesema kuwa tunataka nchi yetu tujivunie bidhaa zinzozalishwa nchini kwa kuhamasisha kila mwananchi kupenda na kununua bidhaa Bidhaa za Tanzania kwa sasa zinakubalika Supermarket nyingi kwa kuwa zinakidhi ubora kupitia TBS na TFDA, aliongeza kwa kusema kuwa Kiwanda ni uongezwaji thamani kutoka malighafi na kuwa bidhaa ambapo Lengo la Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ni kuwa na Viwanda vingi vizalishe bidhaa bora ili tuuze katika masoko ya ndani na nje ya nchi. Mhe. Waziri amesema kuwa Wawekezaji na Wafanyabiashara kujifunza na kuzoea kufanya uwekezaji unaokubalika kisheria (Legal Business Practices) fuateni taratibu za nchi, kulipa kodi zinazowahusu na kuzalisha bidhaa bora na Serikali itasaidia kurahisha shughuli zao. Pia Mhe. Waziri amehimiza Matumizi ya Teknolojia kwa maendeleo ya biashara ambapo amesema ni muhimu kwa wawekezaji hasa wa ndani kwenda sambamba na mahitaji ya teknolojia katika kuzalisha na kuuza bidhaa. Mhe. Waziri amemaliza kwa kusema kusema kuwa Serikali imewekeza nguvu kubwa kwa SIDO katika ujenzi wa Viwanda nchi nzima ambapo Wizara inapokea changamoto mbalimbali zinazokwamisha biashara zao na kuzifanyia kazi kupitia anuani ya dawatilamsaada@mit.go.tz Mhe. Waziri ataendelea na ziara yake kesho Tarehe 3 Januari, 2018 katika Mkoa wa Geita.

Hatimiliki © wizara ya viwanda, biashara na uwekezaji 2019. Haki zote zimehifadhiwa.