Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji

Hon. Charles John Mwijage (MP)

Wasifu

Serikali yasaini makubalino ya kuitoa nchi katika mpango wa nchi kitaifa kwenda kwenye mpango wa nchi na washirika.


Imewekwa: 08th March, 2018

SERIKALI imesaini makubaliano ya kuitoa nchi katika mpango wa nchi kitaifa kwenda kwenye mpango wa nchi na washirika. Lengo la makubaliano hayo ni nchi kufikia uchumi wa kati kupitia uchumi wa viwanda hadi 2025. Hayo yamesemwa Dar es Salaam leo mara baada ya kutiliana saini makubaliano hayo baina ya Waziri wa Viwanda na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage na Mkurugenzi Mkuu wa UNIDO, Li Yong. Makubaliano hayo yamefanyika na kushuhudiwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri wa Mambo ya nje, Balozi Agustino Mahiga na Waziri Mwijage. Akizungumza leo jijini Dar es Salaam mara baada ya kutiliana saini, Waziri Mwijage amesema mpango huo umeshaanza kutumika nakwamba utaiwezesha nchi kufikia uchumi wa kati. "UNIDO ni shirika la umoja wa mataifa linaloshughulikia maendeleo ya viwanda.....sisi kwa kuwa nae inatuweka kwenye nafasi nzuri ya kututafutia wateja...,"amesema. Amesema wanategemea UNIDO kutafuta washirika wengine kwenye mpango wa miaka mitano wa ujenzi wa uchumi wa viwanda ili wasaidie nchi namna ya kutekeleza. Ameongeza kuwa katika mpango wao wa miaka mitano ni kuleta ushindani na nakwamba wataweka miundombinu wezeshi ili kurahisisha kupitisha bidhaa kwa gharama nafuu, upatikanaji wa umeme wa uhakika. "Tunapotafuta na kuandaa wataalamu wetu yeye atatusaidia kufundisha wafungashaji,"amesema. Mwijage amesema watashirikiana nae lengo likiwa kuongeza ajira na kuongeza thamani ya bidhaa na kuongeza pato la taifa na mtu mmoja mmoja. "Lengo la uchumi wa viwanda ni kutengeneza mambo makuu matatu,moja kutengeneza ajira, kuzalisha bidhaa zenye viwango vya hali ya juu na kukidhi mahitaji ya watu na kuuza nje tupate fedha za kigeni na kuwapatia watu kipato, "amesema. Amesema kuongeza kipato kitawafanya wananchi kulipa kodi na hatimaye kuingia kwenye uchumi wa kati. Amesema wataboresha mazingira yauwekezaji huku akiwataka wananchi kulipa kodi. Kwa upande wake Li Yong amesema wapo tayari kufanya kazi na kwamba watalinda mazingira ya viwanda hapa nchini. Ameongeza kuwa wanatambua kuwa takwimu zimeonesha kuna vijana wengi hivyo watatengeneza ajira nyingi kwa vijana ili kukuza uchumi.

Hatimiliki © wizara ya viwanda, biashara na uwekezaji 2018. Haki zote zimehifadhiwa.