Wizara ya Viwanda na Biashara

Waziri wa Viwanda na Biashara

Hon. George Joseph Kakunda (Mb)

Wasifu

KATIBU MKUU VIWANDA AFANYA ZIARA NCHINI BANGLADESH


Imewekwa: 07th February, 2018

Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Prof. Elisante Ole Gabriel atembelea kiwanda cha Madawa cha BEXIMCO kilichopo Dhaka nchini Bangladesh akiwa ameambatana na wajumbe kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki pamoja na wadau kutoka Sekta binafsi. Ziara hiyo ya siku tatu ina lengo la kutafuta wawekezaji, kuongeza ushirikiano na kubadilishana uzoefu na Teknologia. Akiwa katika ziara hiyo Prof. Elisante alisema wamejifunza mambo mengi ikiwemo teknologia ya kisasa inayotumika katika kuzalisha madawa. “nchi ya Bangladeshi imepiga hatua kubwa katika uzalishaji wadawa ukilinganisha na Tanzania,hivyo tumekuja mahali hapa kuangalia wenzetu wanafanyaje katika Sekta hii”. alisema kuwa Tanzania inatumia pesa nyingi kuagiza madawa kutoka nje ya nchi hivyo basi moja ya lengo la ziara hiyo hiyo ni kuangalia fursa na kuwashawishi wawekezaji waliowekeza katika viwanda vya madawa kuja kuwekeza Tanzania. “Tunaamini kwamba viwanda hivi vikija kuwekeza Tanzania tutakuwa tumehimiza uchumi wa Viwanda Katika sekta ya madawa na pia Vijana wetu wengi wataweza kupata ajira“ . Ziara hiyo ya siku tatu imejumuisha wajumbe kutoka Tanzania, Kenya, na Burundi.

Hatimiliki © wizara ya viwanda na biashara 2019. Haki zote zimehifadhiwa.