Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji

Hon. Charles John Mwijage (MP)

Wasifu

Kamati ya kudumu ya Bunge Viwanda, Biashara na Mazingira yakutana na Mhe. Manyanya Iringa.


Imewekwa: 19th March, 2018

Kamati ya kudumu ya Bunge Viwanda, Biashara na Mazingira yakutana na Mhe. Manyanya Iringa. Kamati ya kudumu ya Bunge Viwanda, Biashara na Mazingira yakutana na Mhe. Naibu Waziri wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji na ku[pokea taarifa ya SIDO Iringa. katika taarifa yao SIDO wameeleza shughu;li mbali mbali wanazofanya hasa katika kusaidia wajasiriamali na wafanyabiashara kwa kuwapa elimu, miko[po yenye riba nafuu na ujuzi. Baada ya kupokea taarifa hiyo kamati ya bunge ilitembelea eneo la SIDO Iringa na kujionea shughuli mbalimbali za uzalishaji zinazofanywa kiwandani hapo na kutembelea kiwanda cha Darsh ambacho pia walisaidiwa katika ubunifu wa baadhi ya mashine kiwandani hapo lakini pia SIDO ndio waliohusika katika ushawishi wa uanzishwaji wa kiwanda hiko ili kusaidia waku;lima wa nyanya. Kamati ya bunge imeishauri Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji kufanya juhudi kubwa kusaidia shirika hili la SIDO kwani ndio nguzo pekee kuelekea uchumi wa Voiwanda hivyo ni lazima kusaidiwa kupata teknolojia za kisasa ili kusaidia wajasiriamali kuzalisha bidhaa bora.

Hatimiliki © wizara ya viwanda, biashara na uwekezaji 2018. Haki zote zimehifadhiwa.